Home Sports KAGERA SUGAR KUJA KWA MPANGO HUU

KAGERA SUGAR KUJA KWA MPANGO HUU

KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amefichua kuwa kwa sasa kikosi chake kinaendelea na mazoezi ikiwa ni baada ya kuanza vibaya kwenye michezo yao ya Ligi Kuu Bara.

Baada ya kucheza mechi mbili haijakusanya pointi huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi sita kibindoi.

Yanga pia kwenye mechi mbili za ligi wametupia jumla ya mabao 10 kibindoni.

Kagera imeanza vibaya katika ligi baada ya kupoteza mechi zake dhidi ya Mashujaa FC kwa mabao 2-0 na Ihefu 1-0.

Maxime amesema: “Ni kweli tumeanza vibaya Ligi Kuu Bara nimewahimiza wachezaji wangu na kuwaambia waongeze umakini wakiwa uwanjani.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na Kila mchezaji ana morali na kile ambacho tunafanya mazoezini.

“Nawaandaa wachezaji kiakili na kuwapa fitinesi kwa ajili ya kujihakikishia  wanapambana na kushinda mechi zote na kujiweka kwenye nafasi nzuri.”

Previous articleMAKUNDI UEFA NI KAZIKAZI, ARSENAL VIBONDE
Next articleTFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU WAZIRI WA MICHEZO NDUMBARO