Home Sports MRITHI WA MIKOBA YA HANS PLUIJM SINGIDA FOUNTAIN GATE HUYU HAPA

MRITHI WA MIKOBA YA HANS PLUIJM SINGIDA FOUNTAIN GATE HUYU HAPA

NI Ernst Middendorp raia wa Ujerumani ametangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate.

Anachukua mikoba ya Hans Pluijm ambaye alipewa mkono wa asante rasmi Agosti 29 2023.

Kocha huyo aliwahi kuifundisha Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ikiwa ni miongoni mwa timu ambazo alizifundisha katika bara la Afrika hivyo ana uzoefu na soka la ushindani.

Baada ya kutambulishwa ndani ya Singida Fountain Gate ameweka wazi kuwa anatambua kazi haitakuwa nyepesi lakini ni muhimu kushirikiana.

“Ninatambua kuhusu ligi ya Tanzania na ushindani wake ulivyo mkubwa hivyo ni muda wa kufanya kazi kwa umakini kufikia mafanikio,”

Previous articleVIDEO: ISHU YA KASI YA YANGA KWENYE LIGI SIMBA YAFUNGUKIA HIVI
Next articleMAKUNDI UEFA NI KAZIKAZI, ARSENAL VIBONDE