Home Sports DUBE MGUU KWA MGUU NA JEAN BALEKE

DUBE MGUU KWA MGUU NA JEAN BALEKE

PRINCE Dube, nyota wa Azam FC anakula sahani moja na Jean Baleke wa Simba kwenye suala la utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 tuzo ya ufungaji bora ilikwenda kwa Saido Ntibanzokiza wa Simba na Fiston Mayele wa Yanga.

Mastaa wote wawili wana rekodi ya kufungua akaunti za kutupia mabao katika mechi zao za kwanza kwenye dakika zenye mfanano ikiwa ni rekodi yao ya kwanza na ile ya pili kila mmoja katupia kwenye mechi mbili mfululizo.

Dube alianza kufungua akaunti ya mabao kwenye mchezo dhidi ya Kitayosce uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ni dakika ya tano alipachika bao lake la kwanza.

Ngoma ilijibiwa na Baleke wa Simba aliyefunga bao la kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu ilikuwa dakika ya tano.

Kwenye mchezo wa pili, Baleke alifunga dhidi ya Dodoma Jiji mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru na alipachika bao hilo dakika ya 43 ikiwa ni bao lake la pili kwenye mechi mbili mfululizo.

Dube hakuwa mnyonge alijibu mapigo kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Azam Complex alipachika bao la pili ilikuwa dakika ya 11.

Nyota wote wawili kibindoni wana mabao mawili yote wakiwa wametupia kipindi cha kwanza ndani ya msimu mpya wa 2023/24.

Kwenye msimamo Azam FC ni nafasi ya pili huku vinara wakiwa ni Yanga wakati Simba ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Yanga wanaongoza kwa idadi kubwa ya maao ya kufunga ambayo ni 10 huku Azam FC ikiwa imefunga mabao saba na Simba mabao sita.

Previous articleSIMBA INASUKWA UPYA KITAIFA NA KIMATAIFA
Next articleBEKI WA KAZI KAMILI SIMBA KIMATAIFA