SIMBA YAWAFUNGUKIA AL AHLY

BAADA ya droo ya African Football League kuchezwa na Simba kupangwa kuanza na Al Ahly ya Misri, uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa wapo tayari kuonyesha ukubwa wao.

Simba katika African Football League itaanza na Al Ahly katika hatua ya robo fainali mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Oktoba 20,2023 na ule wa marudiano itakuwa ni Oktoba 24.

Ikiwa Simba itapenya nusu fainali basi itakutana na mshindi kati ya Petro Atletico ama Mamelodi Sundowns.

“Tunashukuru kupangiwa Al Ahly Kwa kuwa katika michuano hii ilikuwa hamna namna ya kuwakwepa, anaitambua Simba tunamkaribisha

Mashabiki waanze kufanya maandalizi ya kununua tiketi mapema kwa sababu mashindano haya yatakuwa na wageni kutoka sehemu mbalimbali, nasi tutaanza kuuza tiketi mapema,”.

Ni timu nane ambazo zinashiriki mashindano haya makubwa Afrika ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika.

Kwenye mechi ya ufunguzi inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kutakuwa na viongozi mbalimbali kutoka CAF na FIFA.