MAXI NAMBA 7 WA YANGA ATUMA UJUMBE HUU KIMATAIFA

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Maxi Mpia
Nzegeli ameweka wazi kuwa malengo yake ni
kuhakikisha kuwa anaisaidia timu hiyo kufanya
vyema katika michuano ya kimataifa na kufikia
malengo yao ya kufika hatua ya makundi.

Yanga ili wafanikiwe kutinga katika hatua ya
makundi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawaondoa Al Merrikh katka mchezo
unaofuata wa hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa
Afrika.

Maxi amesema kuwa
malengo yake ni kuhakikisha anaisaidia Yanga
kufika kwenye malengo kwenye michuano hiyo
kwa kufika katika hatua ya makundi huku
akiamini kuwa wana uwezo mkubwa wa
kuwaondoa Al Merrikh.

“Malengo ya timu ndio malengo ya wachezaji
wote, kwetu sisi tunatamani kuona tukifika
katika makundi na kupita zaidi ya hapo,
kikubwa kwetu tunachokifanya kwa sasa ni
kuona tunajikita zaidi katika kufanya vyema
katika michezo yetu.

“Michezo yetu miwili iliyopo mbeleni dhidi ya Al
Merrikh ni muhimu zaidi kwa upande wetu kuona tunafanya vyema na kupata matokeo,
tunaamini tunao uwezo huo na tutapambana
zaidi kufikia hayo malengo.”