MASTAA YANGA WAPIGWA STOP NA GAMONDI

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi raia
Argentina ni kama amewashtukia wapinzani
wao katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Merrikh
ya Sudan kwa kuamua kufuta mapumziko kwa
wachezaji wa timu hiyo na kuingia kambini na
kuanza maandalizi kuelekea katika mchezo huo.

Yanga ambao imeanza msimu huu kwa
mafanikio kutokana na kutoa vipigo vizito
katika Ligi Kuu Bara pamoja na Ligi ya
Mabingwa Afrika ambapo kwa sasa wapo
kwenye mapumziko ya wiki mbili kwa ajili ya
kupisha michezo ya kuwania kufuzu fainali za
mataifa Afrika (Afcon) zinazotarajia kufanyika
nchini Ivory Coast.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inatarajia
kucheza mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya
kuwania kufuzu katika makundi ya michuano
hiyo, Septemba 16, mwaka huu kabla ya
mchezo wa marudiano unaotarajia kupigwa
Septemba 30, mwaka huu jijini Dar.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo,
zinaeleza kuwa Gamondi amegomea wachezaji
kwenda kukaa mapumziko katika kipindi hiki cha kupisha michezo ya timu za taifa kutokana
na ratiba ngumu iliyokuwepo mbele yao.

Kocha huyo ambaye anatajwa aliwapa siku
moja pekee kwa ajili ya mapumziko kabla ya
juzi wachezaji kurejea kambini kwa wale ambao
hawajaitwa timu za taifa na kuendelea na
program ikiwa ni lengo la kujiandaa na mchezo
huo.

Kwa upande wa Gamondi amesema; “Hakuna sababu ya kupumzika, tayari tulipumzika siku moja na tayari turejea uwanjani, tunatakiwa kufikia malengo yetu hivyo ni vyema tukaongeza nguvu katika kipindi hiki kuhakikisha tunafikia malengo yetu,” amesema Gamondi.