
HASIRA ZA KICHAPO KWA SIMBA KUWAANGUKIA TABORA UNITED
BAADA ya kupoteza kwenye mchezo wao uliopita wa ligi dhidi ya Simba hasira za Coastal Union zinahamia kwa Tabora United unaotarajiwa kuchezwa leo Septemba 29. Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Coastal Union ilifungwa mabao 3-0 ikiwa ugenini dhidi ya mnyama Simba. Mabao yote ya Simba yalifungwa na Jean Baleke ikiwa ni hat trick…