Home International LIVERPOOL BADO WANAJITAFUTA HUKO

LIVERPOOL BADO WANAJITAFUTA HUKO

LIVERPOOL wamekuwa wakijitafuta kwa muda na sasa wanaonekana kurejea kwenye makali yao hiyo ni baada ya wikiendi iliyopita kutoka nyuma na kushinda mabao 3-1 dhidi ya Wolves 3-1 ugenini huko Molineux.

Msimu uliopita ilikuwa mara ya kwanza kwa Liverpool kushindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo Kocha Mkuu Jurgen Klopp amekuwa kwenye usukani kwa msimu mzima. Lakini klabu imejibu kwa kutengeneza nafasi kubwa kwenye kikosi, hasa katika idara ya kiungo.

Majogoo walimaliza msimu uliopita wakiwa katika hali nzuri na walianza pale walipoishia baada ya kuwaingiza Alexis Mac Allister, Dominik Szoboszlai, Wataru Endo na Ryan Gravenberch kwenye safu mpya ya kiungo ya Klopp.

Hapa kuna takwimu 10 zinazoonyesha kuwa Liverpool msimu huu imeanza kurudi kwenye levo zake baada ya mechi tano za kwanza msimu huu ambapo rekodi zinaonyesha wameshinda nne, sare moja na hawajapoteza.

Kwa upande wa mabao, Liver wamefunga 12 na kuruhusu manne pekee hivyo wana alama 13 na wapo nafasi ya tatu huku kinara akiwa Man City wenye pointi 15.

Hizi hapa ni takwimu 10 zinazoonyesha jinsi Liverpool walivyo kwenye njia sahihi ya kurejea katika ubora wao:

 Ni Manchester City na Arsenal pekee ndio wamechukua pointi zaidi ya Liverpool katika kipindi cha kalenda ya mwaka.

Liverpool wamechukua pointi 52 kutoka kwenye michezo 27 mwaka huu. Imeongezwa kwa msimu mzima wa michezo 38, ambayo ina wastani wa pointi 73 – ambayo inakupa uhakika wa kumaliza walau nne bora.

 Liverpool bado walipambana licha ya kupoteana mwanzoni mwa miezi ya 2023, lakini mabadiliko halisi yanaweza kubainishwa pale Klopp alipomhamisha Trent Alexander-Arnold katika nafasi ya kiungo Aprili, kuanzia mchezo wa sare ya 2-2 dhidi ya Arsenal.

Tangu wakati huo, wamechukua pointi 37 kwenye mechi 15 za Ligi Kuu. Ni Man City pekee (pointi 40) walio na rekodi bora zaidi katika kipindi husika.

 Vijana wa Klopp hawajafungwa katika mechi 16 zilizopita za ligi (ushindi 11, sare tano). Ikiwa ni unbeaten ndefu zaidi kwenye Premier.

 Liverpool walipoteza 3-0 walipoenda ugenini kwa Wolves msimu uliopita. Kikosi cha Klopp tayari kimevuna pointi tano za ziada ikilinganishwa na msimu uliopita, baada ya kuifunga Aston Villa 3-0 Uwanja wa Anfield kabla ya ligi kusimama (walitoka sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Villa msimu uliopita).

 Liverpool tayari wamevuna pointi nyingi na ushindi zaidi ya walivyopata kutokana na mechi sita za mwanzo. Msimu uliopita walitoka sare tatu na kupoteza tatu kati ya sita za mwanzoni.

 Salah amehusika kufunga au kutoa asisti kila baada ya dakika 72 msimu huu. Mshambuliaji huyo raia wa Misri, amefunga mabao mawili na kutoa asisti mbili katika mechi tano zilizopita. Amehusika kwenye mabao kwenye kila mchezo ambao Liver wamecheza 2023-24.

Ni Pedro Neto pekee ndiye mwenye asisti nyingi (nne) na Erling Haaland pekee ndiye aliye na mchango zaidi wa mabao (mabao sita, asisti moja) kumzidi Salah.

Salah amerudi kwenye ubora wake. Msimu uliopita alifunga au kuasisti katika mechi 11 zilizopita za Premier League. Mwamba huyu mwenye miaka 31, amefunga mabao 16 na asisti 14 katika mechi 32 za Liverpool mwaka huu.

Ni Manchester City pekee wameruhusu mabao machache zaidi Premier msimu huu hadi sasa. Liverpool wana clean sheet moja, lakini wameruhusu zaidi ya bao moja kwenye kila mechi msimu huu.

Liverpool walitokea nyuma na kushinda katika mechi tatu kati ya tano walizocheza msimu huu.

 

Previous articleZANA ZA KAZI ZAANDALIWA YANGA NA GAMONDI
Next articleNTIBANZOKIZA NA LUIS NDANI YA SIMBA KUNA NAMNA