Home International NTIBANZOKIZA NA LUIS NDANI YA SIMBA KUNA NAMNA

NTIBANZOKIZA NA LUIS NDANI YA SIMBA KUNA NAMNA

VIUNGO wawili wa Simba, Luis Miquissone na Saido Ntibanzokiza chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kuna namna wanazidi kuiva chungu kimoja kutokana na muunganiko wao kuanza kujibu.

Nyota hao kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 6 mwendo wa mpira wa kona iliyopigwa na Luis dakika ya 74 ileleta bao la pili.

Katika mchezo huo Luis alipiga kona kwa kumpa pasi Ntibanzokiza ambaye alijaza krosi iliyokutana na Fabrince Ngoma aliyepachika bao la pili dakika ya 75 kwa pigo la kichwa.

Ngoma ilijibu kwa mara nyingine kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamo uliochezwa Rwanda ni mpira wa kurushwa wa Ntibanzokiza ulikutana na Luis aliyempa pasi ya bao Chama.

Chama alipachika bao hilo la pili dakika ya 90 na ubao ukasoma Power Dynamos 2-2 Simba. Katika mechi walizocheza dhidi ya Power Dynamos mapigo yao yalijibu.

Previous articleLIVERPOOL BADO WANAJITAFUTA HUKO
Next articleAFCON 2027 KUANDALIWANA NCHI TATU, KENYA, UGANDA NA TANZANIA