Home Sports AFCON 2027 KUANDALIWANA NCHI TATU, KENYA, UGANDA NA TANZANIA

AFCON 2027 KUANDALIWANA NCHI TATU, KENYA, UGANDA NA TANZANIA

RASMI mataifa matatu yataandaa mashindano makubwa Afrika ambayo ni Africa Cup.

Mapema Septemba 27, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Damas Ndumbaro aliongozana na ujumbe wa pamoja wa Tanzania, Uganda na Kenya ambapo walikuwa kwenye kikao cha kuwasilisha wasilisho la kuomba kuwa mwenyeji wa AFCON 2027.

Kikao hicho cha CAF ExCO kilifanyika katika hotel ya Marriott, Cairo Misri.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika, (CAF) limepitisha ombi la pamoja la Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa fainali hizo.

Rais wa CAF, Patrice Motsepe ametangaza kuwa AFCON 2027 itachezwa katika nchi hizo tatu jambo lililoleta furaha Kwa viongozi wa Soka kutoka nchi hizo.

Previous articleNTIBANZOKIZA NA LUIS NDANI YA SIMBA KUNA NAMNA
Next articleVIDEO:WASIOMTAKA KOCHA SIMBA WAAMBIWA WASEPE