MCHEZO wa Ligi ya Mabingwa ukiwa ni wa sita kwa wawakilishi wa Tanzania Yanga wapo ugenini nchini Misri dhidi ya Al Ahly.
Dakika 45 za mwanzo timu zote zimetoshana nguvu kwa kuhushudia ubao ukisoma Al Ahly 0-0 Yanga.
Kwenye safu ya ushambuliaji Yanga imeanza na Kennedy Musonda pamoja na Joseph Guede mwamba aliyefunga bao lililoifungulia safari ya kutinga hatua ya robo fainali mazima Yanga mchezo wao uliopita.
Mshindi wa mchezo wa leo Machi Mosi anafungua ukurasa wa kuwa kinara jumlajumla katika kundi D.