Home Sports ZANA ZA KAZI ZAANDALIWA YANGA NA GAMONDI

ZANA ZA KAZI ZAANDALIWA YANGA NA GAMONDI

KUELEKEA mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Al Merrikh, Waarabu hao wa Sudan watakutana na balaa jipya linalosukwa na Miguel Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.

Gamondi anaandaa zana za kazi kuelekea mchezo huo muhimu kwa Yanga kupata ushindi kukata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Afrika.

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar, utatoa mshindi wa jumla atakayekata tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi amesema kila mchezo una mbinu tofauti kulingana na aina ya wapinzani jambo linalofanya wabadili mara kwa mara.

“Kila mchezo una mbinu zake kulingana na aina ya wapinzani ambao tunakutana nao kwani wapinzani wetu wanatupa kazi ya kufanya kwa ajili ya mchezo wetu.

“Kikubwa ambacho tunahitaji ni kuona tunapata matokeo chanya hilo lipo wazi kwani hata wachezaji wenyewe furaha yao ni kuona timu inashinda,” amesema.

Previous articlePOWER DYNAMOS KUPELEKWA AZAM COMPLEX, WATATU WA SIMBA KUWAKOSA
Next articleLIVERPOOL BADO WANAJITAFUTA HUKO