Home Sports POWER DYNAMOS KUPELEKWA AZAM COMPLEX, WATATU WA SIMBA KUWAKOSA

POWER DYNAMOS KUPELEKWA AZAM COMPLEX, WATATU WA SIMBA KUWAKOSA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrikd dhidi ya Power Dynamos ambapo watatumia Uwanja wa Azam Complex.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema hawatakuwa na hamasa kubwa kutokana na Uwanja wa Azam Complex kuwa na uwezo wa kubeba watu 7,000.

Mchezo dhidi ya Power Dynamos utachezwa siku ya Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ally amesema wameamua kucheza saa 10 sababu michezo mingi hapa karibuni walicheza muda huo.

“Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio utafuatiliwa zaidi Afrika kwa wikiendi hii kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Ukubwa wa Simba SC ndio unafanya mchezo huo uwe mkubwa zaidi.

“Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui.

“Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo.

“Tiketi za mzunguko ni Tsh. 10,000, VIP B ni Tsh. 30,000 na Platinum ni Tsh. 150,000 ambayo utapata zawadi, usafiri, chakula ukiwa uwanjani. Watu wanasema Chamazi ni mbali lakini watu wa Platinum Chamazi sio mbali maana wana basi na escort,” amesema Ally.

Previous articleTUSIJUMUISHE USHABIKI KWENYE MASUALA YA KUUMIZWA KWA INONGA
Next articleZANA ZA KAZI ZAANDALIWA YANGA NA GAMONDI