KOCHA AL MERRIKH: YANGA INAOGOPESHA

KOCHA wa Al Merrikh, Osamah Nabieh amekiri kwa kusema kuwa Yanga ni moja kati ya timu ambayo inahofiwa kwa sasa barani Afrika kulingana na kile ambacho inakionyesha ndani ya uwanja haswa kutokana na kupata matokeo mazuri na kucheza mpira mzuri.

Kocha huyo anayokumbukumbu ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 wakiwa nyumbani katika mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Merrikh wanatarajiwa kurudiana na Yanga katika mchezo wa mzunguko wa pili wakiwa ugenini katika Uwanja wa Azam Complex mchezo huo unatarajiwa kufanyika Septemba 30.

“Yanga ni timu kubwa ambayo inawachezaji wenye uzoefu nina amini kwamba uwezo wao wa kucheza mechi nyingi za kimataifa zinawafanya wawe na uimara.

“Haina maana kwamba tuna hofu nao tutajitahidi kutafuta matokeo kwenye mchezo ujao tutakapokutana uwanjani,”.

Kwenye mchezo uliopita Rwanda, ubao ulisoma Al Merrekh 0-2 Yanga ambapo beki Bakari Mwamnyeto alikosekana kwenye mchezo huo kutokana na matatizo ya kifamilia.

Tayari Nondo amerejea kwenye kikosi cha Yanga na kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo huo.