AZAM FC WANA JAMBO LAO

KOCHA Mkuu wa Azam FC Yusuph Dabo amesema kuwa watafanyia kazi makosa yaliyopita kwenye mchezo wao dhidi ya Singida Fountain Gate ili kuendelea kupata ushindi.

Katika mchezo huo Azam FC ilipata bao la ushindi dakika ya 90 kupitia kwa nyota wao Idd Suleiman, (Nado) alimtungua kipa wa Singida Fountain Gate, Beno Kakolanya.

Singida Fountain Gate iliyeyusha pointi tatu mazima kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na hadhi ya ushindani kwa timu zote mbili.

Timu hiyo imeanza maandalizi kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Dodoma Jiji unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Oktoba 3.

Dabo amesema kuwa kwenye mchezo wao dhidi ya Singida Fountain Gate walikutana na ushindani mkubwa kwenye kupata matokeo.

“Ulikuwa mchezo mgumu dhidi ya Singida Fountain Gate mwisho tulipata ushindi hivyo kazi yetu ni kuelekea kwenye mchezo ujao tunaamini tutafanya kazi kubwa kwa mechi zijazo.

“Kushindwa kupata matokeo kwenye kipindi cha kwanza inatufanya tuendelee kutafuta matokeo mpaka mwisho wa mchezo,”