Home Uncategorized AZAM FC WANA JAMBO LAO

AZAM FC WANA JAMBO LAO

YUSUPH Dabo, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa wachezaji wake wote ni muhimu kuendelea kupambana kwenye mechi zote ili kuwapa burudani mashabiki na kupata matokeo chanya.

Timu hiyo mchezo wake uliopita ilikomba pointi tatu mazima dhidi ya Singida Fountain Gate kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Dabo ameweka wazi kuwa bado wachezaji wanaonyesha juhudi kwenye kutimiza majukumu yao licha ya kuwa na makosa madogo ambayo ni muhimu kufanyiwa kazi.

“Wachezaji wanajituma kwenye kutimiza majukumu kutokana na kupata matokeo lakini ni muhimu burudani ikaendelea kwenye mechi zote ambazo tutacheza.

“Kila mchezo unapokwisha tunapata muda wa kufanyia kazi makosa jambo ambalo linazidi kutufanya tuwe imara tuna amini tutakuwa bora na kupata matokeo kwenye mechi ambazo tutacheza,”

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi tisa na vinara ni Yanga nao kibindoni wana pointi tisa.

 

Previous articleSIMBA YAWAVUTIA KASI POWER DYNAMOS LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Next articleCHAMA GARI LIMEWAKA HUKO