FIFA na New Jersey Wakosana Kuhusu Gharama za Usafiri wa Mashabiki Kabla ya Kombe la Dunia 2026
Mgogoro umeibuka kati ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na viongozi wa jimbo la New Jersey nchini Marekani kufuatia ongezeko kubwa la nauli za usafiri wa treni kuelekea mechi za Kombe la Dunia 2026. Ripoti zinaeleza kuwa nauli ya safari ya treni kati ya Penn Station jijini New York na Uwanja wa MetLife ulioko New…