Djigui Diarra kamili kuwakabili Mbeya City

MLINDA mlango namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra ni ruksa kuwakabili Mbeya City kwenye mchezo ujao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Aprili 16, 2026 Uwanja wa KMC Complex.

Kipa huyo alifungiwa mechi 3 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) kutokana na kosa la utovu wa nidhamu alilofanya mchezo wa ligi, Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC.

Tayari mechi 3 zimepita kwa mabingwa hao watetezi hivyo ni rasmi atakuwa huru kurejea uwanjani kwa mechi zijazo.

Hizi hapa mechi ambazo alikosekana Diarra:-

Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons, Uwanja wa KMC Complex, Aprili 4, 2026.NBC Premier League

 Pamba Jiji FC 0-3 Yanga SC, Uwanja wa Kirumba, Aprili 8, 2026. NBC Premier League

Yanga SC 1-0 TMA Stars, Aprili 11, 2026, Uwanja wa KMC Complex. CRDB Federation Cup

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.