Jonathan Sowah arejeshwa Simba SC

Jonathan Sowah amerejeshwa katika kikosi cha Simba SC kwa masharti afanye mazoezi na timu ya vijana chini ya miaka 20, (Simba SC U 20) Sowah raia wa Ghana alisimamishwa Februari timu ilipokuwa inajiandaa kuikabili Dodoma Jiji FC. Alikosekana kwenye mechi za ushindani ikiwemo mchezo wa Kariakoo Dabi, Yanga SC 0-0 Simba SC.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema mchezaji huyo alifika mbele ya kamati ya nidhamu ya klabu na kupatikana na hatia kwa baadhi ya makosa yaliyokuwa yakimkabili. Aliongeza kuwa kamati imeamua Sowah afanye mazoezi na timu ya vijana chini ya uangalizi wa karibu. Kurejea kikosi cha wakubwa itategemea na mwenendo wake.

“Kwa sasa Sowah bado ni mchezaji wetu na anatakiwa kufanya mazoezi na timu ya U20. Hii ni sehemu ya mchakato wa kumfuatilia na pindi kamati itakaporidhika na tabia yake, atarejea kwenye kikosi cha wakubwa,”.

Mchezo ujao kwa Simba SC ni Aprili 15, 2026 vs Fountain Gate.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.