KMC FC vs Tanzania Prisons ni balaa zito leo ndani ya NBC Premier League inayotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex, saa 1:00 usiku.
Utamu wa mechi ya leo unanogeshwa na vita yakupambana kushuka daraja kwa timu zote mbili ambapo wenyeji KMC FC wanaburuza mkiwa wakiwa na pointi 8 kwenye msimamo wa ligi.
Tanzania Prisons ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 13 zote mbili zimecheza mechi 18 hivyo atakayeshinda leo anaongeza pointi kujinasua hapo alipo.
KMC FC haijawa kwenye mwendo mzuri ndani ya msimu mpya ikiwa inaongoza kufungwa magoli mengi ambayo ni 29.
Timu hiyo inaongoza kwa kufungwa kwenye mechi nyingi ambazo ni 14 inakutana na mpinzani ambaye amepoteza jumla ya mechi 11.
Kwenye eneo la ushindi KMC FC imepata ushindi mechi 2 huku wapinzani Tanzania Prisons wakiwa wamepata ushindi kwenye mechi 3.
Mchezo uliopita ikiwa ugenini KMC FC ilipoteza kwa kufungwa goli 1-0 dhidi ya Singida Black Stars, Uwanja wa Airtel.
.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.