Fountain Gate vs Simba SC

Fountain Gate vs Simba SC ni mchezo unaofuata kwenye ratiba kwa wababe hawa kusaka pointi 3 ndani ya dakika 90.

Fountain Gate kwenye msimamo ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 16 baada ya mechi 17 ipo kwenye mstari wa kucheza play off.

Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 36 baada ya mechi 17 msimu wa 2025/26.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha saa 10:00 jioni.

Issa Mbuzi Ofisa Habari wa Fountain Gate amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na watapambana kupata pointi 3 muhimu.

“Tupo tayari kuwakabili wapinzani wetu Simba SC kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu tukiwa nyumbani. Mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia burudani na mchezo mzuri,”.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.