Fountain Gate 0-3 Simba SC ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa leo Aprili 15, 2026 NBC Premier League Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Mchezo wa leo ulianza kwa kasi katika dakika 44 za mwanzo ambapo Fountain Gate walikuwa wakijilinda zaidi na Simba SC ikitafuta goli la kuongoza.
Ni kiungo Clatous Chama alifunga goli la kwanza dakika ya 45+7 akitumia makosa ya Jimson Mwanuke aliyekuwa akiokoa hatari kuelekea langoni mwao.
Libasse Gueye alifunga goli la pili dakika ya 53 kwa pasi ya Seleman Mwalimu na kamba ya tatu ni Shaban Mgunda alijifunga dakika ya 71 alipokuwa akiokoa hatari langoni mwa Fountain Gate.
Matokeo haya yanaifanya Simba SC kufikisha pointi 39 nafasi ya pili kwenye msimamo vinara ni Yanga SC wenye pointi 44 tofauti ya pointi 5 na timu zote zimecheza mechi 18.
Fountain Gate ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 16 baada yakucheza mechi 18 msimu wa 2025/26.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.