

SIMBA YABADILISHA RATIBA YA LIGI KUU
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko machache kwenye ratiba ya Ligi Na ya NBC yakiathiri tarehe za michezo 12, muda wa kuanza kwa michezo sita na kuipangia tarehe michezo mitatu ambayo haikuwa na tarehe kwenye ratiba ya awali pamoja na rmchezo wa kiporo kati ya Kagera Sugar na Simba SC. Mabadiliko hayo yamelenga…

HATMA YA KOCHA WA AZAM FC BAADA YA KUTINGA FAINALI NI HII
MABOSI wa Azam FC wameweka wazi kuwa kwa sasa hawana hesabu za kuachana na kocha wao wa muda Abdihamid Moallim,’Master’ raia wa Somalia. Kocha huyo ni Mmarekani mwenye asili ya Simalia aliibuka Azam FC na kupewa majukumu ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha Kukuza Vipaji cha Azam FC, (Azam Academy). Kwa sasa amepwa…

ISHU YA PHIRI KUIBUKIA YANGA IPO HIVI
MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amefunguka kuwa suala la mshambuliaji wa Zanaco, Moses Phiri kujiunga na timu hiyo kwa kusema ni suala la muda kwa kuwa linashughulikiwa kwa weledi mzuri. Yanga inapambana kunasa saini ya mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 17 msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Zambia. Habari zinaeleza kuwa Yanga ipo kwenye mazungumzo na mshambuliaji huyo ili kuweza kumuongeza…

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatano

IKIWA NA MOHAMED SALAH, MISRI YAPIGWA AFCON
NIGERIA wameipoteza Misri katika mchezo wa Kombe la Mataifa ya Afrika,’Afcon,’ ambapo baada ya dakika 90 ubao wa Roumde Adjia ulisoma Nigeria 1-0 Misri. Licha ya uwepo wa staa anayekipiga ndani ya Liverpool, Mohamed Salah, Misri ilikwama kupata ushindi kwenye mchezo huo. Bao la ushindi kwa Nigeria iliyo kundi D lilifungwa na Kelechi Iheanacho dakika…

VIDEO:KUMBE SIMBA WALIWAANDALIA YANGA MCHEZO MKUBWA
AHMED Ally, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa walicheza mchezo mkubwa mbele ya Namungo na wanaomba radhi kwa mchezo huo kwa kuwa waliandaa mchezo huo kwa ajili ya watani zao Yanga ambao wametolewa kwa kupoteza wa kufungwa penalti 9-8 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu. Ameongeza kuwa wanahitaji Kombe hilo na wanawatambua Azam FC lakini…

VIDEO:MASTAA YANGA WALEJEA DAR,SIMBA WAWAPOKEA
MASTAA wa Yanga ambao walikuwa wanashiriki Kombe la Mapinduzi pamoja na viongozi leo Januari 11 wamerejea Dar wakitokeza Zanzibar ambapo walikuwa na kazi ya kutetea Kombe la Mapinudzi ila walivuliwa na Azam FC baada ya kupoteza kwenye changamoto ya penalti. Baada ya dakika 90 kwenye mchezo huo ubao wa Uwanja wa Amaan ulisoma Azam FC…

SAKHO ACHEKELEA KUTINGA FAINALI
PAPE Sakho, kiungo mshambuliaji ndani ya kikosi cha Simba amesema kuwa kwake ni furaha kuona timu hiyo inatinga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi. Jana Januari 10, Sakho alikuwa ni miongoni mwa nyota walioanza kikosi cha kwanza mbele ya Namungo FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya pili. Simba ilishinda mabao 2-0…

MASTAA YANGA WAREJEA DAR WAKITOKEA ZANZIBAR
BAADA ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi jana Januari, 10,2022 leo wamewasili Dar wakitokea Zanzibar. Yanga iliyokuwa inatetea Kombe la Mapinduzi iliishia hatua ya nusu fainali ambapo ilipoteza kwa changamoto ya penalti dhidi ya Azam FC. Dakika 90 zilikamilika kwa timu kutoshana nguvu bila kufungana ugumu ukawa kwenye penalti ambapo Azam ilishinda penalti 9-8…

KIUNGO DENNIS NKANE AWEKWA CHINI YA UANGALIZI
KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Denis Nkane ni kama ameanza vibaya ndani ya timu hiyo baadaya mapema tu kupata uvimbe juu ya goti la kulia na kumfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda, huku akiwekwa chini ya uangalizi maalum wa daktari. Nkane ni kati ya wachezaji wanne waliosajiliwa na kutambulishwa ndani ya Yanga katika usajili huu wa dirishadogo uliofunguliwa Desemba 16, 2021 na kutarajiwa kufungwa Jumamosi hii. Wachezaji…

MFUNGAJI BORA KOMBE LA MAPINDUZI HAYUPO
JANUARI 11,2021 kiungo Miraj Athuman, ‘Sheva’ akiwa ndani ya Simba alifunga bao lake la nne katika Kombe la Mapinduzi. Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 2-1 na Sheva aliibuka kuwa mfungaji bora. Mwaka 2022 atakuwa kwa kideo akishuhudia tuzo yake ikisepa kwa kuwa kwa sasa anakipiga KMC kwa kuwa hayupo katika mashindano hayo mwaka huu…

KIUNGO WA SIMBA KUIBUKIA DTB,TAMBWE KUONGEZEWA NGUVU
OFISA Mtendaji Mkuu wa DTB, Muhibu Kanu ameweka wazi kuwa wapo kwenye mpango wa kuongeza nguvu kwa upande wa safu ya ushambuliaji ili kumuongezea nguvu mshambuliaji Amiss Tambwe. Kwa sasa timu hiyo ipo kwenye mchakato wa mwisho wa kumtangaza James Kotei ambaye ni kiungo mkabaji na aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba. Ndani ya…

VIDEO:KIPA ALIYEFUNGWA NA SAKHO ATAJA KILICHOWAFANYA WAKAFUNGWA
JANA Januari 10, Namungo FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi na kuwafanya wafungashiwe virago kwa kuishia hatua ya nusu fainali, Nahimana ambaye ni kipa aliokota mabao mawili yalifungwa na Sakho pamoja na Meddie Kagere ambao waliweza kufunga kwenye mchezo huo.

AZAM FC WABABE MBELE YA SIMBA
REKODI zinaonyesha kwamba Azam FC wametwaa Kombe la Mapinduzi mara nyingi kuliko mpinzani wake Simba. Hivyo Azam FC ni wababe mbele ya Simba kwenye Kombe la Mapinduzi kila wanapokutana kwenye mchezo wa fainali. Azam FC imetwaa taji la Kombe la Mapinduzi mara tano huku Simba ikiwa imetwaa Kombe la Mapinduzi mara tatu. Hii inakuwa ni…

BIG MATCHES KURINDIMA VIWANJANI! NANI NI NANI?
Burudani ya soka la Afrika inaendelea. AFCON 2022, Nusu fainali ya EFL Cup sambamba na Super Cup nchini Hispania kutoa mchongo wa wiki. Meridianbet mambo yapo hivi; Nigeria watairusha karata yao ya kwanza kwenye mashindano ya AFCON dhidi ya Mafarao wa Misri. Kelechi Iheanacho uso kwa uso na Mo Salah! Ni nani atayaanza…

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE
Spoti Xtra Jumanne, ukurasa wa mbele Januari 11,2022.