>

SIMBA YABADILISHA RATIBA YA LIGI KUU

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imefanya mabadiliko machache kwenye ratiba ya Ligi Na ya NBC yakiathiri tarehe za michezo 12, muda wa kuanza kwa michezo sita na kuipangia tarehe michezo mitatu ambayo haikuwa na tarehe kwenye ratiba ya awali pamoja na rmchezo wa kiporo kati ya Kagera Sugar na Simba SC.

Mabadiliko hayo yamelenga kuepuka uwepo wa michezo ya viporo kutokana na ushiriki wa Simba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) huku michezo mitatu ikipangiwa tarehe baada ya kufaharnika kwa hatma ya ushiriki wa klabu nne (Yanga, Simba, Azam na Namungo) katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Ratiba ya awali ya Ligi Kuu ya NBC ilizingatia ushiriki wa klabu nne (Sirnba, Yanga, Azam na Biashara United) kwenye michuano ya CAF kwa kuzipatia nafasi ya kutosha kwa ajili ya maandalizi, safari na kucheza mechi za michuano hiyo nyumbani na ugenini.

Kuondolewa kwa klabu za Yanga, Azam na Biashara United kwenye michuano ya CAF, kumeilazimu Bodi ya Ligi kupitia upya ratiba ya Ligi na kufanya mabadiliko haya iii Ligi iendelee kuchezwa bila kuwa na mechi za viporo kwa timu yoyote ikiwerno Simba ambayo inaendelea na mashindano hayo.
tff

Jedwali lifuatalo limeainisha mabadiliko hayo kwa kina;
Advertisement

18/12/2021 kuchezwa 26/01/2022, Kagera vs Simba

14/01/2022 kuchezwa 17/01/2022, Polisi Tanzania vs Namungo

16/01/2022, Costal Union vs Yanga

18/01/2022, Mbeya Kwanza vs Azam

17/01/2022, Mbeya City vs Simba

05/02/2022 kuchezwa 03/02/2022, Ruvu Shooting vs Mbeya Kwanza

06/02/2022 kuchezwa 03/02/2022, Simba vs Mbeya Kwanza

23/02/2022 kuchezwa 22/02/2022, Biashara United vs Azam

02/03/2022 kuchezwa 03/03/2022, Simba vs Biashara United

03/03/2022 kuchezwa 27/02/2022, Yanga vs Kagera Sugar

03/03/2022 kuchezwa 01/03/2022, Azam vs Costal

05/03/2022 kuchezwa 07/03/2022, Simba vs Dodoma Jiji

06/03/2022 kuchezwa 04/03/2022, Kagera vs Namungo

06/03/2022 kuchezwa 05/03/2022, Azam vs Polisi Tanzania

15/03/2022 kuchezwa 27/03/2022, Polisi Tanzania vs Simba