AZAM FC YATAMBA KUIFUNGA SIMBA FAINALI
BAADA ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa penalti 9-8 dhidi ya Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi, uongozi wa Azam umetamba kuwa utaibuka na ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Simba na kuandika rekodi mpya kwenye michuano hiyo. Hii inakuwa ni mara ya sita Azam kucheza fainali ya Kombe la Mapinduzi ambapo wamekuwa na rekodi nzuri katika michuano hii, wakifanikiwa kushinda fainali tano zilizopita. Kwenye historia ya michuano hiyo Azam na Simba zimefanikiwa kukutana katika fainali tatu…