KESHO NI FAINALI YA KISASI

HII ni fainali ya kisasi ikiwa kutanisha Simba dhidi ya Azam, katika mchezo utakaopigwa kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Ni fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa msimu wa 16. Azam imebeba ubingwa huo mara tano, huku Simba ikibeba mara tatu.

Timu hizi zinakwenda kukutana katika fainali ya nne kwenye michuano hii, baada ya mara tatu zote Azam FC kuibuka na ushindi Fainali ya kisasi mwaka 2012, 2017 na 2019 ambayo ilikuwa mara ya mwisho kwao kukutana.

Jumatatu, Azam FC ilikuwa ya kwanza kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Yanga kwa penalti 9-8, huku Simba ikija kuifunga Namungo mabao 2-0 yaliyofungwa na Meddie Kagere dakika ya 15 na Pape Sakho dakika ya 49.


Azam na Simba 
tangu mara ya mwisho kupambana ndani ya Ligi Kuu Bara na Simba kushinda 2-1. Ilikuwa Januari Mosi, mwaka huu.