>

SIMBA YALIPIGIA HESABU KOMBE LA YANGA

OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, kuelekea fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC. inayotarajiwa kupigwa Kesho Januari 13 Uwanja wa Amaan lengo lao namba moja ni kuweza kusepa na kombe hilo ambalo lilikuwa mikononi mwa Yanga.

Ni Yanga walikuwa wanatetea Kombe la Mapinduzi walitolewa na Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa Amaan kwa changamoto ya penalti ambapo Azam FC ilishinda penalti 9-8 ilikuwa ni kwa upande wa Yanga.

Katika mchezo wa nusu fainali dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-0 Yanga jambo lililofanya mshindi asakwe kwa changamoto ya penalti.

Rasmi sasa Azam FC kesho itamenyana na Simba iliyotinga hatua ya fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo FC ambayo nayo tayari imesharejea Dar jana Januari 11 kama ilivyokuwa kwa Yanga.

Ally amesema:”Furaha yetu ni kuona kwamba tunashinda mchezo wetu na tupo imara kwa ajili ya mchezo wetu wa fainali ambao tunaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa lakini tunahitaji kutwaa Kombe la Mapinduzi.

“Kuanzia kwa wachezaji achana na Pape Sakho ambaye ni mchezaji mzuri na alipewa tuzo kwenye mchezo wetu dhidi ya Namungo ile ni tuzo ya wachezaji wote kwa kuwa walicheza vizuri kazi yetu sasa ni kuheza fainali na Azam FC ambao walishinda kwa penalti, kikubwa ni kusubiri na kuona namna itakavyokuwa,”.

Yanga ilitwaa Kombe la Mapinduzi 2021 kwa ushindi wa penalti 5-3 dhidi ya Simba mchezo uliochezwa Januari 13,2021 zama hizo ilikuwa na nahodha Haruna Niyonzima.