MABOSI wa Azam FC wameweka wazi kuwa kwa sasa hawana hesabu za kuachana na kocha wao wa muda Abdihamid Moallim,’Master’ raia wa Somalia.
Kocha huyo ni Mmarekani mwenye asili ya Simalia aliibuka Azam FC na kupewa majukumu ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha Kukuza Vipaji cha Azam FC, (Azam Academy).
Kwa sasa amepwa majukumu ya kuinoa Azam FC ile ya wakubwa baada ya George Lwandamina kubwaga manyanga ya kuinoa timu hiyo.