Home Sports KIUNGO WA SIMBA KUIBUKIA DTB,TAMBWE KUONGEZEWA NGUVU

KIUNGO WA SIMBA KUIBUKIA DTB,TAMBWE KUONGEZEWA NGUVU

OFISA Mtendaji Mkuu wa DTB, Muhibu Kanu ameweka wazi  kuwa wapo kwenye mpango wa kuongeza nguvu kwa upande wa safu ya ushambuliaji ili kumuongezea nguvu mshambuliaji Amiss Tambwe.
Kwa sasa timu hiyo ipo kwenye mchakato wa mwisho wa kumtangaza James Kotei ambaye ni kiungo mkabaji na aliwahi kucheza ndani ya kikosi cha Simba.
Ndani ya Championship, DTB ipo nafasi ya kwanza imekusanya pointi 36 baada ya kucheza mechi 14 na ni Gwambina inashikilia nafasi ya 16 na pointi zake ni sita.
Kwa upande wa safu ya ushambuliaji DTB imefunga jumla ya mabao 27 na mshambuliaji wa kwanza kufunga mabao alikuwa ni Tambwe aliyeweza kufunga hat trick ya kwanza mbele ya African Lyon Uwanja wa Uhuru na DTB ilishinda mabao 4-1.
Kanu amesema:”Tunahitaji kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu kwa kuwa malengo yetu ni kuleta ushindani wa kweli kwenye ligi ambayo ina ushindani mkubwa.
“Kikubwa ni kuangalia namna ripoti ya mwalimu ambavyo itakuwa inasema sisi hatuna tatizo tunafuata kile ambacho kimesemwa,” amesema.
Previous articleVIDEO:KIPA ALIYEFUNGWA NA SAKHO ATAJA KILICHOWAFANYA WAKAFUNGWA
Next articleMFUNGAJI BORA KOMBE LA MAPINDUZI HAYUPO