KIUNGO DENNIS NKANE AWEKWA CHINI YA UANGALIZI

KIUNGO mshambuliaji mpya wa Yanga, Denis Nkane ni kama ameanza vibaya ndani ya timu hiyo baada
ya mapema tu kupata uvimbe 
juu ya goti la kulia na kumfanya kuwa nje ya uwanja kwa muda, huku akiwekwa chini ya uangalizi maalum wa daktari.

Nkane ni kati ya wachezaji  wanne waliosajiliwa na kutambulishwa ndani ya Yanga katika usajili huu wa dirisha
dogo uliofunguliwa Desemba 
16, 2021 na kutarajiwa kufungwa Jumamosi hii.

Wachezaji wengine waliosajiliwa na Yanga ni Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Crispin Ngushi na Aboutwalib Mshery.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassani Bumbuli, alisema Nkane aliukosa mchezo wa jana Jumatatu wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC baada ya kupata majeraha hayo.

Bumbuli alisema kiungo huyo alipata majeraha katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM uliomalizika kwa sare ya 2-2.


“Nkane baada ya kupata 
majeraha, amepewa mapumziko maalum huku akiwa chiniya uangalizi wa madaktari wanaoendelea kumpatia matibabu yatakayomrejesha uwanjani mapema.


“Sure Boy amepata malaria 
akiwa huku Zanzibar, naye amepewa mapumziko maalum huku akiendelea na matibabu yatakayomresha uwanjani haraka,” alisema Bumbuli.