
SIMBA YAICHAPA TATU DODOMA JIJI NA KUSEPA NA POINTI TATU
JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema ushindi ambao wameupata kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji umetokana na kazi kubwa ya wachezaji wakeo uwanjani. Baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 3-0 Dodoma Jiji na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 13 na kuongoza ligi. Bao la ufunguzi lilifungwa na Abdallah Shaibu,’Ninja’…