Home Uncategorized NABI ATAMBA NA WACHEZAJI WAKE WA KAZI

NABI ATAMBA NA WACHEZAJI WAKE WA KAZI

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zote za kitaifa na kimataifa kutokana na uwepo wa wachezaji wenye uwezo.

Mchezo ujao Yanga unatarajiwa kuchezwa Oktoba 3,2022 utakuwa wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting na kete yao inayofuata kimataifa itakuwa dhidi ya Al Hilal, Uwanja wa Mkapa, Oktoba 8,2022.

Miongoni mwa mastaa ambao wanatarajiwa kuwa kwenye kikosi cha Yanga, Jumatatu ni pamoja na Aziz KI ambaye amesharejea kambini pia kiraka Yannick Bangala naye yupo kambini.

Ki raia wa Burkina Faso ndani ya Bongo kwenye ligi katupia bao moja na ana pasi moja ya bao pia, ni mbele ya Mtibwa Sugar waliposhinda mabao 3-0 alifunga Uwanja wa Mkapa.

Nabi amesema:”Kila mchezaji anajituma katika kutimiza majukumu ikiwa ni pamoja na Aziz KI, Fiston Mayele, kila mchezaji anafanya kazi kubwa hilo ni jambo la muhimu.

“Kikubwa ni maandalizi na kila mchezaji anajituma kwenye kutimiza majukumu yake,” .

Previous articleMANAHODHA SIMBA NA DODOMA JIJI TAMBO TUPU
Next articleARSENAL YAMOTO, YAICHAPA SPURS 3-1