Home Sports MANAHODHA SIMBA NA DODOMA JIJI TAMBO TUPU

MANAHODHA SIMBA NA DODOMA JIJI TAMBO TUPU

MOHAMED Hussein, nahodha msaidizi wa Simba amesema wapo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Dodoma Jiji.

Huo ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkapa.

Beki huyo amebainisha kwamba wanatambua ukubwa wa Dodoma Jiji kweye ushindani hivyo watajitahidi kutafuta ushindi.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji tunawatambua wapinzani na tunawaheshimu hivyo ni suala la kuona mashabiki wanajitokeza kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” amesema.

Kibacha Mbwana nahodha wa Dodoma Jiji amebainisha kuwa wachezaji watajituma na wanahamu ya kucheza na timu kubwa ambayo ni Simba.

Previous articleSAUTI:KOCHA IBENGA AWA MPOLE, KISA REKODI YAKE UWANJA WA MKAPA
Next articleNABI ATAMBA NA WACHEZAJI WAKE WA KAZI