Home Sports DAKIKA 180 ZAIPA NGUVU SIMBA KUIKABILI DODOMA JIJI

DAKIKA 180 ZAIPA NGUVU SIMBA KUIKABILI DODOMA JIJI

DAKIKA 180 ambazo Simba imezitumia kwenye mechi za kirafiki Zanzibar zimewapa nguvu ya kupambana dhidi ya Dodoma Jiji.

Leo kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kitatupa kete yake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mgunda amesema kuwa mechi mbili ambazo wamecheza Zanzibar zinawapa nguvu kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji

“Mechi mbili ambazo tumecheza zimetupa nguvu kuelekea kwenye mechi yetu dhidi ya Dodoma Jiji, kikubwa ni kuona tunapata pointi tatu na wachezaji wapo tayari kutimiza wajibu wao.

“Mchezaji Jimmson Mwanuke alipata maumivu lakini tunasubiri ripoti kutoka kwa madaktari, wachezaji wengine wapo tayari kwa ajili ya kutafuta ushindi na tunawaheshimu wapinzani wetu,” amesema Mgunda.

Mohamed Hussein, nahodha msaidizi wa Simba amebainisha kuwa wapo tayari kwa mechi yao dhidi ya Dodoma Jiji.

Previous articleSUALA LA MZUNGU WA SIMBA LIWE SOMO KWA WENGINE
Next articleYANGA WAPIGA HESABU KUMALIZA KAZI MAPEMA KIMATAIFA