Home Uncategorized YANGA WAPIGA HESABU KUMALIZA KAZI MAPEMA KIMATAIFA

YANGA WAPIGA HESABU KUMALIZA KAZI MAPEMA KIMATAIFA

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga ameweka wazi kuwa kweye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hawadharau wapinzani wao na badala yake wanahitaji ushindi dakika za mwanzo.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi inakibarua cha kusaka ushindi Ligi ya Mabingwa raundi ya Pili dhidi ya Al Hilal mchezo unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 8, Uwanja wa Mkapa.

Imetinga hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 9-0 dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini na mechi zote hizo zilichezwa Uwanja wa Mkapa.

Kaze amesema: “Kwenye mechi za kimataifa ambazo tunacheza ni muhimu kwetu kupata ushindi dakika za mwanzo ili kuongeza hali ya kujiamini na kuwa kwenye mchezo.

“Tutajitahidi kupata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza na maandalizi ni mazuri kuanzia kwenye saikolojia ya wachezaji pamoja na utimamu wao.

“Hatuwezi kudharau timu hata moja ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika, benchi la ufundi na wachezaji tunaongeza umakini na kusahihisha makosa ambayo yamepita kwenye mechi zetu,” .

Previous articleDAKIKA 180 ZAIPA NGUVU SIMBA KUIKABILI DODOMA JIJI
Next articleVIDEO: HII HAPA MBINU YA DODOMA JIJI KUIMALIZA SIMBA KWA MKAPA