Timu ya Taifa ya Canada itamenyana na Uzbekistan leo Juni 2 saa 04:00 alfajiri katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa kwenye Uwanja wa Commonwealth mjini Edmonton.
Mchezo huu ni sehemu muhimu ya maandalizi ya mataifa hayo kuelekea Kombe la Dunia 2026, huku Canada ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo pamoja na Marekani na Mexico.
Canada chini ya kocha Jesse Marsch imekuwa ikionyesha maendeleo makubwa katika miaka ya karibuni, ikicheza soka la kasi na presha kubwa uwanjani. Kikosi hicho kina nyota kama Jonathan David, Tajon Buchanan na Stephen Eustaquio, lakini kimekumbwa na changamoto za majeraha baada ya kiungo Marcelo Flores kuumia ACL huku nahodha Alphonso Davies akiwa bado hajarejea katika kiwango chake kamili kutokana na majeraha ya misuli.
Kwa upande wa Uzbekistan, timu hiyo imeendelea kukua kisoka na imekuwa moja ya mataifa yenye ushindani mkubwa barani Asia. Wana wachezaji wenye uzoefu kama Eldor Shomurodov, Jaloliddin Masharipov na Otabek Shukurov ambao wana uwezo wa kuibadilisha mechi kwa kasi kupitia mashambulizi ya kushtukiza na matumizi mazuri ya mipira ya mwisho.
Ingia kwenye kasi ya kujishindia pesa kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kiufundi, Canada wanaonekana kuwa na faida ya kucheza nyumbani pamoja na ubora wa safu yao ya ushambuliaji. Takwimu zinaonyesha kuwa wamefungwa bao moja au chini yake katika mechi 13 kati ya 14 zilizopita huku wakitunza clean sheet mara tano katika michezo sita ya hivi karibuni. Hata hivyo, Uzbekistan wameonyesha uimara mkubwa wa kujilinda na wamekuwa wagumu kufungwa katika mechi zao za karibuni za kirafiki.
Matarajio makubwa ni kuona pambano lenye ushindani mkali kutokana na timu zote mbili kuwa katika maandalizi ya hatua muhimu za kimataifa. Canada wanaonekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na ubora wa kikosi na faida ya uwanja wa nyumbani, lakini Uzbekistan wana uwezo wa kusababisha mshangao kama watatumia vizuri nafasi za mashambulizi ya kushtukiza. Mashabiki wanatarajia mchezo wa kuvutia wenye kiwango cha juu cha ushindani.