SUALA LA MZUNGU WA SIMBA LIWE SOMO KWA WENGINE

    IMESHATOKEA mwanzoni kabisa msimu wa 2022/23 wakati wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika Simba wakiwa kwenye maandalizi.

    Tukio ambalo kila kiongozi analishangaa kwa nini limetokea na kwa nini imekuwa hivyo wakati ambao hawakutarajia.

    Ni kweli kwa namna ilivyotokea lazima kila mmoja atapambana kuonyesha kwamba hakutarajia kuona inatokea ilihali ukweli unajulikana.

    Mkataba wao ambao waliingia na mshambuliaji Dejan Georgijevic tayari umevunjwa kwa kile kilichoelezwa kuwa kuna masuala ya kimkataba hayakufuatwa.

    Hili sio jambo geni kuona linatokea lakini kwenye soka letu la hapa Bongo imekuwa ni nadra sana mchezaji kueleza kwamba makubaliano yake kimkataba hayajafuatwa.

    Kwa kilichotokea Simba ni somo kwa timu nyingine kwamba wapo wachezaji ambao wanatazama kila kipengele katika utekelezaji wake.

    Hawa ni wale wenye kiu ya mafanikio na wanaamini katika makubaliano ila kama ni kweli Dejan aliamua kukimbilia kwenye mitandao na kuzungumza suala hilo hapo kuna makosa kwa pande zote mbili.

    Huenda mabosi wa Simba hawakutaka kuzungumza naye bali walitaka kukamilisha masuala hayo kishkaji jambo ambalo wachezaji wakigeni huwa hawaamini katika hilo wanazingatia makubaliano.

    Timu zetu kwa hili ambalo limetokea ni muhimu kujifunza na kuaandaa mikataba ambayo itakuwa na masharti yanayoweza kufanyika kwa wakati.

    Wachezaji pia kuvunja mikataba kuna utaratibu ambao upo huo ni lazima ufuatwe ili kila mmoja apate haki yake.

    Ikumbukwe kwamba Mzungu huyo alisepa wakati timu ikiwa kambini na ilikuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Kipanga.

    Hili ni somo kwani ingekuwa kwenye mechi ya ushindani na ikatokea timu ikafungwa basi sababu ingetafutwa kuwa wachezaji hawakuwa sawa kisaikolojia.

    Previous articleKIUNGO WA YANGA AZIZ KI KUIKOSA RUVU SHOOTING
    Next articleDAKIKA 180 ZAIPA NGUVU SIMBA KUIKABILI DODOMA JIJI