MICHEZO ISIYO YA KIUNGWANA ISIPEWE NAFASI

KILA siku tunashuhudia ushindani mkubwa kwenye mechi ambazo zinachezwa ndani ya uwanja wa kila timu kupambania kupata ushindi hilo ni jambo la msingi ambalo linapaswa kuwa endelevu.

Wakati haya yanaendelea kumekuwa na tatizo la wachezaji  kuendelea kutumia nguvu nyingi na wakati mwingine kucheza faulo hata pale ambapo haihitajiki kabisa.

Muhimu kuongeza umakini na kuendelea kucheza kwa kufuata sheria 17 za mpira hilo litafanya wanaocheza kutimiza majukumu yao huku kila mmoja akiwa kwenye ubora wake.

Kwa sasa ni muda wa kuendelea kufanyia kazi makosa yaliyopita ili kuwa imara kwa mechi zijazo na inawezekana kwa kuwa muda upo na kikubwa ni kupata ushindi.

Pia kuna umuhimu mkubwa kufanyia maboresho sehemu ya kuchezea kwa kuwa hiyo inatoa picha ya maandalizi ambayo yamefanyika kwa muda.

Hakuna mchezaji anayependa kuona anapata maumivu kutokana na kucheza sehemu ambayo si salama kwake hivyo uboreshaji kwenye eneo la kuchezea ni muhimu kufanyika kwa ajili ya matokeo ya kesho.

Muda uliopo kwa sasa ni kuendelea kufanya mipango mizuri kwaajili ya kukamilisha mzunguko wa kwanza ambao ushindani wake ni mkubwa.

Wachezaji wanatambua namna hali ilivyo hivyo kikubwa ambacho kinatakiwa ni kuona kila mmoja anatimiza majukumu yake kwa wakati pale anapopata nafasi.

Mashabiki nao wasiache kujitokeza uwanjani kushuhudia timu zao zikiwa zinacheza kwa kuwa wanaongeza nguvu kwa wachezaji ndani ya dakika 90 kutafuta ushindi muhimu.

Muda uliopo ni sasa kufanyia kazi makosa yaliyopita na hali hii itaongeza ufanisi na ushindani zaidi kwenye kila idara ndani ya timu.

Kila timu mpango kazi wake ni kupata matokeo hivyo kwa wale ambao hawajawa kwenye mwendo mzuri ni muda wa kufanya maboresho kwenye makosa yaliyopita.

Ipo wazi kwamba kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri lakini kuna wachezaji wanaokwama kuonyesha viwango vyao katika mechi za ushindani.

Kwenye mapambano ya kusaka ushindi ni muhimu kuongeza nidhamu ndani ya uwanja nan je ya uwanja. Hilo litafanya kazi ziende kwa umakini na benchi la ufundi kupata fursa ya kuwatumia wachezaji wote ambao wapo katika kikosi.

Ikiwa wapo watakaokuwa wanakwenda tofauti kwenye maandalizi ya mechi husika ni muhimu kurejea kwenye njia wakati ujao na kufanya kazi kubwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi zinazofuata.

Kwa zile timu ambazo bado zinatambua mwendo wao haujawa mzuri ni muhimu kuangalia pale ambapo wanakosea ili kupata matokeo mazuri kwa mechi zijazo.

Furaha ya mashabiki inahitajika kwa kuwa wanachohitaji wao ni kuona timu inapata matokeo chanya. Kupatikana kwa matokeo mazuri haitokei kawaidani kwa juhudi isiyokuwa ya kawaida kila wakati.

Jambo la msingi kwa mashabiki ni kuamini kwamba dakika 90 zinabeba maamuzi ya matokeo ya uwajani. Kazi yao moja kubwa iwe katika kushangilia bila kuchoka.

Yote kwa yote ni muhimu kila mmoja akatimiza majukumu yake kwa wakati uwanjani na kuongeza ushirikiano hilo litaongeza nguvu ya kupata matokeo mazuri.

Kila la kheri kwenye maandalizi na kazi kubwa iwe katika kuongeza burudani na mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.