Home Sports YANGA YAKAA NAMBA MOJA

YANGA YAKAA NAMBA MOJA

YANGA imeibuka na ushindi wa bao 1-0 Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Bao pekee la ushindi limefungwa na Mudathir Yahya dakika ya 86 akitumia pasi ya Kibabage.

Wakali wote wawili walitokea benchi kipindj cha pili ambapo Dodoma Jiji walikuwa wanakaribia kupata pointi moja mpango ukavurugwa jioni.

Mbinu ya Dodoma Jiji ilikuwa ni kujilinda zaidi n kushambulia kwa kushtukiza Jambo ambalo halijawapa matokeo.

Sasa Yanga inarejea nafasi ya kwanza ikiwashusha Azam FC mpaka nafasi ya pili huku Simba ikiwa nafasi ya tatu.

Ni pointi 34 imekusanya baada ya kucheza mechi 13 sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili na pointi 31 huku Simba ikiwa nafasi ya tatu na pointi 26 baada ya kucheza mechi 11

Previous articleTABORA UNITED YATUMA UJUMBE HUU SIMBA
Next articleMICHEZO ISIYO YA KIUNGWANA ISIPEWE NAFASI