Home Sports KIUNGO MGUMU AMPA TABASAMU MGUNDA SIMBA

KIUNGO MGUMU AMPA TABASAMU MGUNDA SIMBA

JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kurejea kwa kiungo wake wa kazi Sadio Kanoute kwenye kikosi hicho kunaongeza uwanda mkubwa wa kuchagua viungo ambao anawahitaji.

Kanoute raia wa Mali ambaye ni kiungo mgumu kwenye eneo la ukabaji sifa yake kuu ni kutembeza mikato ya kimyakimya alikosekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons kutokana na adhabu ya kadi tatu za njano.

Kiungo huyo anatarajiwa kuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa leo Jumapili, Uwanja wa Mkapa.

 Mgunda amesema kuwa kwa sasa yupo tayari kumtumia Kanoute kwenye mechi zake kwa kuwa adhabu yake imeisha.

“Kanoute amerejea na yupo fiti hasa kwenye mazoezi pamoja na mechi ambazo anacheza anaonyesha kitu cha kipekee, hivyo kurejea kwake kunaongeza chaguo la wachezaji ambao wataanza kwenye kikosi kulingana na namna ambavyo wataamka na ripoti ya daktari,” alisema.

Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Big Bullets, Sadio alitumia dakika 90, alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 60.

Previous articleVIDEO: HII HAPA MBINU YA DODOMA JIJI KUIMALIZA SIMBA KWA MKAPA
Next articleYANGA NI WAKALI KWENYE USHAMBULIAJI