
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu
KIKOSI cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Red Arrows kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90, Kocha Mkuu, Pablo Franco hakuwa na namna ya kufanya kutokana na mazingira ya uwanja kutokuwa rafiki kwa kuwa uwanja…
UWANJA wa Mkapa leo Novemba 28 katika dakika 45 za kwanza Simba wanaongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia. Umakini hafifu wa Simba unawafanya waende chumba cha kubadilishia nguo wakiongoza kwa mabao mawili jambo ambalo linawapa ugumu kuweza kulinda ushindi huo ambao una ushindani mkubwa. Mabao ya Simba yamefungwa na Bernard Morrison…
RASMI kikosi cha Simba kitakachoanza leo dhidi ya Red Arrows , Uwanja wa Mkapa saa 10:00 jioni mchezo wa Kombe la Shirikisho:- Aishi Manula Pascal Wawa Joash Onyango Israel Mwenda Mohamed Hussein Jonas Mkude Hassan Dilunga Sadio Kanoute Meddie Kagere Bernard Morrison Rally Bwalya
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’, Sajenti Seleman Kidunda amefichua kuwa kama kuna bondia anaamini uchawi unasaidia kwenye kupigana basi atamruhusu aende akaloge halafu akakutane na mziki wake. Kidunda hivi karibuni amepandishwa cheo kutoka Koplo hadi Sajenti kwa sasa anajiandaa na pambano lake la ubingwa wa dunia ‘WBF’ dhidi ya Tshimanga Katompa kutoka DR Congo katika Pambano la Usiku wa Mabingwa litakalopigwa Desemba…
BINTI Naima Omary ni mchezaji mzuri wa Basket Ball amebainisha kuwa alianza kupenda mchezo huo akiwa shule na kwa sasa bado anaendelea kipaji chake akiendelea na masomo nchini Uganda.
JOHN Boco nahodha wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Bocco amebainisha kuwa kupoteza mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa kwa kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Jwaneng Galaxy kumewafunza…
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa baada ya kutoa sare katika mchezo uliopita dhidi ya Namungo hawatahitaji matokeo kama hayo katika mchezo unaofuata dhidi ya Mbeya Kwanza zaidi ya ushindi tu. Yanga katika mchezo uliopita walitoa sare dhidi ya Namungo kwa bao 1-1, Novemba 30 wanatarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza mkoani Mbeya. Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa matokeo ambayo waliyapata kwenye mchezo…
KAMA ingekuwa ni utulivu wa mshambuliaji wa Simba Kibu Dennis akiwa ndani ya 18 basi kwa sasa angekuwa yupo kwenye orodha ya wakali wa kucheka na nyavu kutona na nafasi ambazo amekuwa akizipata na kushindwa kuzitumia. Rekodi zinaonyesha kuwa ni jumla ya nafasi tisa za wazi aliweza kutengeneza huku katika nafasi hizo akifunga bao moja…
MOHAMED Makaka kipa namba moja wa Ruvu Shooting anaingia kwenye orodha ya makipa wa kazi chafu kutokana na uwezo wake wa kuokoa mashuti yasiweze kuingia kwenye lango lake. Mastaa wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere bado watakuwa wanajua balaa la mikono yake licha ya Simba kushinda kwa mabao 3-1 bado Makaka alikuwa mhimihili kwa timu…
DIDIER Gomes, aliwahi kuwa kocha mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa kwa namna kikosi hicho kilivyo kinaweza kupata ushindi mbele ya Red Arrows katika mchezo wa Kombe la Shirikisho. Leo Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa mtoano ambao utashuhudiwa na mashabiki 35,000. Gomes amesema kuwa…
IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Borussia Dortmund, Erling Haaland yupo kwenye hesabu za mabosi wa Real Madrid ambao wanawinda saini yake. Ripoti zinaeleza kuwa Haaland mpaka sasa bado hajafanya maamuzi ya wapi atakuwa kwa ajili ya kupata changamoto mpya licha ya timu nyingi kutajwa kuwania saini yake. Winga huyo amekuwa akizivutia timu mbalimbali kutokana…
LEO Novemba 28, Uwanja wa Stamford Bridge kitawaka kwa mchezo mkali wa Ligi Kuu England kati ya Chelsea v Manchester United. Mwamuzi wa kati atakuwa ni Anthony Taylor ambaye akishapuliza kipyenga leo atakuwa anaashiria kuanza kuzitafuta dakika 90 za mchezo wa leo. Chelsea watakuwa nyumbani ambapo wataikaribisha Manchester United na ni vinara wa ligi kwa…
KAZI itakuwa moja kwa Kocha Mkuu, Pablo Franco kuwaongoza vijana wake kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni wa mtoano dhidi ya Red Arrows. Ni leo Novemba 28, Uwanja wa Mkapa mchezo huo unatarajiwa kuchezwa na mashabiki 35,000 wameruhusiwa kuweza kushuhudia mchezo huo. Pablo anatarajia kuwa kwenye benchi la ufundi na kwa…
KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Novemba 28 kimekwea pipa kwa ajili ya kuelekea Mbeya. Ni Air Tanzania itawafikisha Mbeya kwa ajili ya kuweza kuanza kufanya maandalizi ya mwisho baada ya jana Novemba 27 kufanya mmazoezi kwa mara ya mwisho kambini Kigamboni kabla ya leo kusepa. Mchezo wao wa ligi unatarajiwa…
MSIMU wa 2021/22 unazidi kuchanja mbuga mdogomdogo na kwa sasa kuna timu zipo raundi ya 6 na nyingine ni ile ya saba. Msimamo upo namna hii
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Jumapili