Home Sports YANGA YAKWEA PIPA KUWAFUATA MBEYA KWANZA

YANGA YAKWEA PIPA KUWAFUATA MBEYA KWANZA

KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Novemba 28 kimekwea pipa kwa ajili ya kuelekea Mbeya.

Ni Air Tanzania itawafikisha Mbeya kwa ajili ya kuweza kuanza kufanya maandalizi ya mwisho baada ya jana Novemba 27 kufanya mmazoezi kwa mara ya mwisho kambini Kigamboni kabla ya leo kusepa.

Mchezo wao wa ligi unatarajiwa kuchezwa Novemba 30, Jumanne dhidi ya Mbeya Kwanza ,Uwanja wa Sokoine.

Unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa timu hizi kukutana kwa sababu Mbeya Kwanza imepanda daraja msimu huu.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 6 na Mbeya Kwanza wao kibindoni wana pointi 7 baada ya kucheza mechi sita pia.

Previous articleMSIMAMO WA LIGI KUU BARA UPO NAMNA HII
Next articleKIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA RED ARROWS