KAZI itakuwa moja kwa Kocha Mkuu, Pablo Franco kuwaongoza vijana wake kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ni wa mtoano dhidi ya Red Arrows.
Ni leo Novemba 28, Uwanja wa Mkapa mchezo huo unatarajiwa kuchezwa na mashabiki 35,000 wameruhusiwa kuweza kushuhudia mchezo huo.
Pablo anatarajia kuwa kwenye benchi la ufundi na kwa namna ambavyo amekwenda na wachezaji wake kwenye mazoezi inatarajiwa kuanza na wachezaji hawa kikosi cha kwanza:-
Aishi Manula
Pascal Wawa
Hencok Inonga
Shomari Kapombe
Mohamed Hussein
Jonas Mkude
Hassan Dilunga
Rarry Bwalya
John Bocco
Meddie Kagere
Bernard Morrison
Chanzo:Spoti Xtra