Home International LEO KITAWAKA STAMFORD BRIDGE

LEO KITAWAKA STAMFORD BRIDGE

LEO Novemba 28, Uwanja wa Stamford Bridge kitawaka kwa mchezo mkali wa Ligi Kuu England kati ya Chelsea v Manchester United.

Mwamuzi wa kati atakuwa ni Anthony Taylor ambaye akishapuliza kipyenga leo atakuwa anaashiria kuanza kuzitafuta dakika 90 za mchezo wa leo.

Chelsea watakuwa nyumbani ambapo wataikaribisha Manchester United na ni vinara wa ligi kwa sasa wana pointi zao 29 wapinzani wao Manchester United wana pointi 17.

Moja ya mchezo mkali ambapo United itakuwa kazini bila kocha wao Ole ambaye amechimbishwa kikosini hapo watakuwa na kocha wao wa mpito wa Michael Carrick an united kwenye mechi zake 12 imepoteza mechi tano.

Chelsea itaingia ikiwa na nguvu kubwa katika mchezo wa leo saa 1:30 kuendeleza kasi ya kuuwinda ubingwa wa Ligi Kuu England huku Manchester United nao wakiwa wanahitaji pointi tatu muhimu.

 

Previous articleKIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA RED ARROWS
Next articleHAALAND AINGIA ANGA ZA REAL MADRID