HAALAND AINGIA ANGA ZA REAL MADRID

IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Borussia Dortmund, Erling Haaland yupo kwenye hesabu za mabosi wa Real Madrid ambao wanawinda saini yake.

Ripoti zinaeleza kuwa Haaland mpaka sasa bado hajafanya maamuzi ya wapi atakuwa kwa ajili ya kupata changamoto mpya licha ya timu nyingi kutajwa kuwania saini yake.

Winga huyo amekuwa akizivutia timu mbalimbali kutokana na uwezo wake jambo ambalo linafanya kila muda kutajwa kuwa anaweza kuondoka ndani ya kikosi hicho.

Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuwania saini yake mbali na Real Madrid ni pamoja na Barcelona,Chelsea,Manchester United na Manchester City.