Home Sports DAKIKA 90 ZAKAMILIKA SIMBA YASHINDA 3-0 KIMATAIFA

DAKIKA 90 ZAKAMILIKA SIMBA YASHINDA 3-0 KIMATAIFA

KIKOSI cha Simba kimeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Red Arrows kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90, Kocha Mkuu, Pablo Franco hakuwa na namna ya kufanya kutokana na mazingira ya uwanja kutokuwa rafiki kwa kuwa uwanja ulikuwa na maji baada ya mvua kunyesha ila hiyo haikuwa tatizo ushindi ulipatikana.

Nyota wa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji, mzee wa kuchetua Bernard Morrison ambaye alihusika katika mabao yote matatu ambayo yalifungwa ndani ya dakika 90.

Morrison alitupia mabao mawili ilikuwa dakika ya 16 na dakika ya 77 huku moja lilifungwa na Meddie Kagere dakika 19 kwa pasi ya Morrison.

Ingekuwa ni utulivu wa Morrison angefanikiwa kufunga mabao manne kwa kuwa alikosa penalti moja na alikosa nafasi ya wazi moja dakika ya 90 kwa pasi ya Peter Banda.

 

Previous articleDAKIKA 45 SIMBA WATAWALA KWA MKAPA NA KUTUPIA MBILI
Next articleMUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU