>

DAKIKA 45 SIMBA WATAWALA KWA MKAPA NA KUTUPIA MBILI

UWANJA wa Mkapa leo Novemba 28 katika dakika 45 za kwanza Simba wanaongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Umakini hafifu wa Simba unawafanya waende chumba cha kubadilishia nguo wakiongoza kwa mabao mawili jambo ambalo linawapa ugumu kuweza kulinda ushindi huo ambao una ushindani mkubwa.

Mabao ya Simba yamefungwa na Bernard Morrison dakika ya 16 na bao la pili likafungwa na Meddie Kagere dakika ya 19.

Morrison atajilaumu mwenyewe kwa kushindwa kufunga penalti dakika ya 31 baada ya kipa kuikoa ndani ya ya 18.

Penalti hiyo imesababishwa na Hassan Dilunga ambaye alichezewa faulo ndani ya 18 na nyota wa Red Arrows.