Home Sports KIDUNDA AFUNGUKIA KUHUSU UCHAWI KWENYE NGUMI

KIDUNDA AFUNGUKIA KUHUSU UCHAWI KWENYE NGUMI

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’, Sajenti Seleman Kidunda amefichua kuwa kama kuna bondia anaamini uchawi unasaidia kwenye kupigana basi atamruhusu aende akaloge halafu akakutane na mziki wake.

Kidunda hivi karibuni amepandishwa cheo kutoka Koplo hadi Sajenti kwa sasa anajiandaa na pambano lake la ubingwa wa dunia ‘WBF’ dhidi ya Tshimanga Katompa kutoka DR Congo katika Pambano la Usiku wa Mabingwa litakalopigwa Desemba 26, mwaka huu.

Kidunda amesema kwa upande wake hawezi kuwa na imani za kishirikina kuwa msaada kwenye mapambano zaidi ya kufanya makali ambayo yamekuwa msaada kwenye mapambano yake kuweza kushinda.


“Binafsi siwezi kuamini mambo ya 
kishirikina kwamba yanasaidia bondia au mtu kuweza kufanya vizuri katika ngumi yaani nitoke hapa nikaloge ili niweze kushinda hilo jambo kwangu haliwezi kuwezekana, hapa ni mazoezi ndiyo dawa.

“Sasa kama yupo mtu anaamini katika huo uchawi basi mimi namruhusu halafu aje acheze na mimi ataona balaa ambalo litakalomfanyia,” alisema Kidunda.

Chanzo:Championi

Previous articleVIDEO:NAIMA MWANAFUNZI MWENYE KIPAJI
Next articleRASMI KIKOSI CHA SIMBA V RED ARROWS