
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumamosi
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumamosi
RAIS wa Heshima wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji,’Mo’ amesema kuwa wana imani kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane. Jumapili, Simba itakuwa na kazi ya kusaka ushindi mbele ya RS Berkane katika mchezo wa Kombe la Shirikisho unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa. Leo Mo alikuwa anazungumza na…
KOCHA Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema wao ndio watakaokuwa mabingwa mwisho wa msimu hata kama watu hawawapi nafasi. Julio amesema, kila mechi ambayo wanakwenda kuicheza kwa sasa itakuwa ni kama fainali, kwa sababu wanahitaji kupata alama tatu ambazo zitawafanya wawe mabingwa mwisho wa msimu. Namungo wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi,…
KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya RS Berkane, benchi la ufundi la timu hiyo linafanya maandalizi makubwa kuhakikisha si tu kwamba kikosi chao kinaibuka na ushindi dhidi ya Berkane, lakini pia kinatoa burudani ya kibingwa. Simba wanatarajia kuvaana na Berkane keshokutwa Jumapili katika mchezo wao…
KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameonyesha kuwa hataki kufanya mchezo katika suala la kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, hii ni baada ya kuwaambia mastaa wake kuhakikisha wanakuwa na mawazo ya pointi tatu tu, katika mchezo wao ujao dhidi ya KMC. Kuelekea mchezo huo dhidi ya KMC utakaochezwa Jumamosi ijayo, kikosi cha…
Tunaendelea tulipoishia wikiendi iliyopita. Manchester United na muendelezo wa michezo muhimu nap engine yenye kuamua hatma yao msimu huu. PSG nao wamerudishwa kwenye Ligue1, UEFA hawapawezi. Uturuki nako kunapambamoto, SuperLig kwenye ubora wake. Afrika napo mambo ni bambam kunako mashindano ya CAF, usikae mbali na Meridianbet! Izundue wikiendi kwa mchezo wa Mashindano ya CAF…
AISHI Manula, kipa namba moja wa Simba amesema kuwa wanaendelea vizuri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kimataifa dhidi ya RS Berkane. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili Machi 13 na mashabiki wamepewa nafasi ya kuweza kuuona mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Manula amesema kuwa wanatambua wapinzani wao watakuwa…
KATIKA kuwavuruga wapinzani wao katika Ligi Kuu Bara, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi amesema kuwa anahitaji mabao ya ndani ya dakika 10 ili kuweza kujenga hali ya kujiamini. Hiyo ni moja ya mikakati yake mipya atakayokuja nayo mara baada ya kurejea katika ligi watakapovaana dhidi ya KMC Machi 16, mwaka huu…
KIRAKA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco, Erasto Nyoni amesema kuwa wana imani ya kupata pointi tatu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya RS Berkane unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Uwanja wa Mkapa.
KLABU ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunissia kesho, Jumamosi Machi 12 inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Somalia. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya KMC….
MALI za mmiliki wa Klabu ya Chelsea na bilionea wa Kirusi, Roman Abramovich zimezuiliwa rasmi na Serikali ya Uingereza kuanzia, Machi 10, 2022 kama sehemu ya kuwatia kitanzi matajiri wote wa Kirusi ambao wanahusishwa na kuwa na ukaribu na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Abramovich anaingia kwenye orodha ya mabilionea saba wa Urusi waliowekewa vikwazo…
NYOTA wa zamani wa kikosi cha Yanga ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya kikosi cha RS Berkane, Fiston Abdoul Razak ameweka wazi kwamba kikosi chao ni bora kuliko wapinzani wao Simba. Jana, Machi 10 RS Berkane waliwasili Tanzania kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa baada ya kuanza safari Machi 9 wakitokea…
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Ijumaa
BARBARA Gonzalez, Mtendaji Mkuu wa Simba SC, amesema wapinzani wao RS Berkane kwenye mchezo unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Jumapili hii, hawatatoka salama. Simba inatarajiwa kumenyana na RS Berkane ya Morocco kwenye mchezo wa nne wa Kundi D, wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita ugenini kwa kufungwa mabao 2-0. Barbara amebainisha kuwa, kwa maandalizi…
AISHI Manula, ‘Air Manula’ kipa namba moja wa Simba ni Air Manula kwelikweli kama anavyopenda kuitwa kwa kuwa amewafunika makipa wote kwa upande wa kucheza mechi nyingi na kuwa namba moja kufungwa mechi chache. Pongezi kubwa kwa ukuta wa Simba unaongozwa na Joash Onyango pamoja na Henock Inonga ambao umeweza kumshuhudia kipa wao akiokota mabao…
FISTON Mayele, nyota wa kikosi cha Yanga yupo kamili gado kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za ushindani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho. Mayele alipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba. Kwenye mchezo huo Mayele alikwama kuyeyusha dakika 90 na aliweza…
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kwa msimu wa 2021/22 wamekuwa wakipata mateso makubwa ugenini katika msako wa pointi tatu kwa kuwa mambo yamekuwa ni magumu kwao. Kwa mzunguko wa kwanza katika mechi 15 ambazo wamecheza na kuweka kibindoni pointi 31 ni mechi 7 walicheza ugenini na kushinda 3 huku wakiambulia sare 2 na…