HAJI MANARA AWAIBUA WAZAWA WA KAZI CHAFU

HAJI Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo wazawa wengi ambao wanafanya vizuri ndani ya kikosi cha Yanga ikiwa ni pamoja na Dickson Job, Kibwana Shomari pamoja na Feisal Salum. Nyota hao kwa sasa wana uhakika wa namba kikosi cha kwanza ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nasredddine Nabi  huku nahodha akiwa ni mzawa pia…

Read More

KUMBE ILIKUWA NI GHAFLA TU KUMFUTA KAZI NUNO

IMERIPOTIWA kuwa ilikuwa ni ghafla kwa mabosi wa Klabu ya Tootenham kumfuta kazi kocha wao Nuno Espirito ambaye ametangazwa kuwa kwa sasa hatakuwa kwenye majukumu yake ya kazi. Ikumbukwe kwamba Nuno alipokea mikoba ya Jose Mourinho ambbaye alifutwa kazi hapo Aprili 19,2021 kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo. Nuno alichaguliwa kuwa kocha Juni 30,2021…

Read More

BRENDAN HAFIKIRII KUIFUNDISHA MANCHESTER UNITED

BOSI wa Leicester City, Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hafikirii kwenda kuifundisha Manchester United. Rodgers amesisitiza kuwa malengo yake ni kuweza kuona timu yake ya sasa inatwaa mataji zaidi. Kocha huyo amekuwa akitajwa kwenda kuinoa Manchester United ambayo inaweza kumtimua Ole Gunnar Solkjaer. Bosi huyo amesema:”Malengo yangu siku zote ni kuona Leicester inaendelea kuwa bora,kutwaa mataji…

Read More

SPORTPESA NGUZO YA MWENDO WA WAKONGWE YANGA

  NDANI ya miaka minne tu, kampuni maarufu zaidi nchini ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa ndio inayoshikilia rekodi ya kuwa kampuni iliyoweka fedha nyingi zaidi za udhamini katika klabu kongwe zaidi nchini ya Yanga na ndio mabingwa wa kihistoria.   Yanga ndio klabu kongwe na ambayo imechukua makombe mengi zaidi ya Ligi Kuu Bara…

Read More

LIVERPOOL YAMPA KOCHA WAKE HASIRA

KOCHA Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amegeuka mbogo kwa wachezaji wake kwa kuwaeleza kuwa walicheza chini ya kiwango kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England na kuwafanya watoshane nguvu na wapinzani wao Brighton.   Ilikuwa ni Oktoba 30 ambapo Liverpool walikuwa wanapewa nafasi ya kushinda kwa kuwa walikuwa wametoka kuwanyoosha mabao matano Manchester United ila…

Read More

MSIMAMO WA LIGI KUU BARA HUU HAPA

LIGI Kuu Tanzania Bara maarufu kama NBC Premier Ligi inazidi kuchanja mbunga ambapo tayari kuna timu zimeanza kuonja ladha ya kuwa nafasi ya kwanza pamoja na ile ladha ya kuwa nafasi ya mwisho ndani ya msimu wa 2021/22 ambao unakwenda kwa kasi.   Huu hapa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga wakiwa ni namba moja…

Read More

YANGA MACHO KWENYE UBINGWA WA LIGI KUU BARA

BAKARI Mwamnyeto,  nahodha wa Yanga amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.   Yanga ikiwa imecheza mechi nne imeshinda zote na kujiwekea kibindoni pointi zake 12 inashika nafasi ya kwanza huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 6. Wapinzani wao Simba wapo…

Read More

MABINGWA WATETEZI WABANWA MBAVU KWA MKAPA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo Oktoba 31 wamebwana mbavu mbele ya Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara baada ya kugawana pointi mojamoja. Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa ni wa nguvu nyingi imeshuhudiwa ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 0-0 Coastal Union ya kule Tanga. Kadi mbili nyekundu…

Read More

MESSI MAMBO MAGUMU PSG

NYOTA wa kikosi cha PSG, mshambuliaji Lionel Messi mambo kwake ni magumu kwenye ishu ya kucheka na nyavu baada ya kuweka rekodi ya kucheza mechi tano bila kufunga. Ni giza nene limeendelea kutanda kwenye macho yake kwa sasa staa huyo ambaye alikuwa akikiwasha ndani ya Barcelona kwani tayari amecheza mechi hizo ndani ya Ligue 1…

Read More

KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA COASTAL UNION

LEO Oktoba 31 mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba wanatarajia kucheza na Coastal Union kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku. Hiki hapa kikosi cha Simba ambacho kinatarajiwa kuanza leo kwa mujibu wa rekodi za Saleh Jembe:- Aishi Manula Shomari Kapombe Mohamed Hussein Joash Onyango Henock Inonga Mzamiru…

Read More

ARSENAL GARI IMEWAKA HUKO

AARON Ramsdale kipa wa Arsenal aliweza kuwa imara akiwa langoni wakati timu yake iliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Leicester City uliochezwa Uwanja wa King Power. Ilikuwa ni mabao ya Gabriel Magalhaes ilikuwa dakika ya 5 na lile la pili lilipachikwa na Emule Smith Rowe dakika ya 18 na kuipa pointi tatu timu hiyo inayonolewa na…

Read More

KOCHA NABI ATAJWA KUIBUKIA SIMBA

IMEELEZWA kuwa, licha ya Mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, kuachia nafasi ya Uenyekiti waBodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, lakini bado anahusika kwenye baadhi ya mambo ikiwemo kipindi hiki chamchakato wa kusaka kocha mpya wa kuinoa timu hiyo.   Wakati Simba ikiwa kwenye mchakato wa kumsaka mrithi wa Kocha Didier Gomes aliyeachia ngazi Jumanne ya wiki hii, baadhi ya viongozi wa Simba wameonekana kulijadili jina la Kocha…

Read More

HITIMANA AUTAKA UBINGWA SIMBA

HITIMANA Thiery, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba amebainisha kuwa timu hiyo inahitaji kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa ni timu kubwa na inawezekana kutokana na ukubwa wa timu hiyo. Mchezo wa kwanza kukaa kwenye benchi akiwa ni kaimu baada ya Didier Gomes kubwaga manyanga ilikuwa ni mbele ya Polisi Tanzania na Simba ilishinda…

Read More

FEI TOTO APELEKWA ULAYA

KITASA wa zamani wa Yanga ambaye sasa anakipiga ndani ya Polisi Tanzania, Said Juma Makapu, amesema anaamini kwa kiwango alichonacho kiungo wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, ni muda wake sasa kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi. Kwa kusema hivyo kitasa huyo ni kama amempeleka Ulaya kiungo huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye ubora wake ndani ya Ligi…

Read More